Genesis 10:5-11

5(Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.)

Wazao Wa Hamu

6 aWana wa Hamu walikuwa:
Kushi, Misraimu,
Yaani Misri.
Putu na Kanaani.
7 cWana wa Kushi walikuwa:
Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.
Wana wa Raama walikuwa:
Sheba na Dedani.

8 dKushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani. 9 eAlikuwa mwindaji hodari mbele za Bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za Bwana.” 10 fVituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari. 11 gKutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala,
Copyright information for SwhNEN